Jeremiah 51:37-42


37 aBabeli utakuwa lundo la magofu
na makao ya mbweha,
kitu cha kutisha na kudharauliwa,
mahali asipoishi mtu.

38 Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo,
wanakoroma kama wana simba.

39 bLakini wakati wakiwa wameamshwa,
nitawaandalia karamu
na kuwafanya walewe,
ili wapige kelele kwa kicheko,
kisha walale milele na wasiamke,”
asema Bwana.

40 “Nitawateremsha kama wana-kondoo waendao machinjoni,
kama kondoo dume na mbuzi.


41 c“Tazama jinsi Sheshaki
Sheshaki ni Babeli kwa fumbo.
atakamatwa,
majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa.
Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi gani
kati ya mataifa!

42 eBahari itainuka juu ya Babeli;
mawimbi yake yenye kunguruma yatamfunika.
Copyright information for SwhKC